+ -

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَبْلَ وَفَاتِهِ بِثَلَاثٍ يَقُولُ:
«لَا يَمُوتَنَّ أَحَدُكُمْ إِلَّا وَهُوَ يُحْسِنُ بِاللهِ الظَّنَّ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2877]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufa kwake kwa siku tatu akisema:
"Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2877]

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza muislamu kuwa asife isipokuwa katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu kwa kuwa na matarajio makubwa ya kheri wakati wa kufikwa na mauti kuwa Mwenyezi Mungu atamhurumia na kumsamehe, kwa sababu hofu hutakiwa kwa ajili ya kufanya vizuri katika matendo, na katika hali hiyo si hali ya kufanya amali yoyote, kinachotakiwa hapo nikuwa na matumaini makubwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Pupa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuuelekeza umma wake, na huruma yake kubwa kwao katika hali zake zote; hata katika maradhi ya kifo chake unaunasihi umma wake na anauelekeza katika njia za kuokoka.
  2. Amesema Attwaibi: Fanyeni matendo yenu kuwa mazuri hivi sasa ili dhana yenu iwe nzuri kwa Mwenyezi Mungu wakati wa kifo, kwani yatakayekuwa mabaya matendo yake kabla ya kifo chake atakuwa na dhana mbaya wakati wa kufa kwake.
  3. Hali kamili ya mja nikuwa kati ya matumaini na hofu, na mapenzi makubwa; mapenzi ndio kipando, na matumaini ndio gurudumu, na hofu ndio mwendo, na Mwenyezi Mungu ndiye mfikishaji kwa neema zake na karama zake.
  4. Inalazimu kwa atakayekuwa karibu na aliyefikwa na mauti azidishe kwake kumpa matumaini na kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, katika hadithi hii Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameyasema haya kabla ya kufa kwake kwa siku tatu.