+ -

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لاَ تَتَّخِذُوا الضَّيْعَةَ فَتَرْغَبُوا فِي الدُّنْيَا».

[حسن لغيره] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 2328]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Msitengeze mabustani, mkajakuipenda sana dunia".

[Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyingine] - - [سنن الترمذي - 2328]

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kujitengenezea makonde na mabustani na mashamba; kwa sababu hilo ni katika sababu za kuipenda sana dunia na kubweteka nayo na kuisahau Akhera.

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kukithirisha sana hadhi za kidunia kwa sababu hupelekea kuiacha Akhera.
  2. Katika hadithi hakuna katazo la kutengeneza yale yanayopelekea maisha, bali katazo ni kuzama katika dunia na kuisahau Akhera.
  3. Amesema Sanadi: Na makusudio yake: Nikuwa msizame katika kutengeneza mabustani, mkapumbazika nayo na mkajisahau kumtaja Mwenyezi Mungu.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama