عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: بَلَغَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم عَنْ أَصْحَابِهِ شَيْءٌ، فَخَطَبَ فَقَالَ:
«عُرِضَتْ عَلَيَّ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَلَمْ أَرَ كَالْيَوْمِ فِي الْخَيْرِ وَالشَّرِّ، وَلَوْ تَعْلَمُونَ مَا أَعْلَمُ لَضَحِكْتُمْ قَلِيلًا وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيرًا» قَالَ: فَمَا أَتَى عَلَى أَصْحَابِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمٌ أَشَدُّ مِنْهُ، قَالَ: غَطَّوْا رُءُوسَهُمْ وَلَهُمْ خَنِينٌ، قَالَ: فَقَامَ عُمَرُ فَقَالَ: رَضِينَا بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا، قَالَ: فَقَامَ ذَاكَ الرَّجُلُ فَقَالَ: مَنْ أَبِي؟ قَالَ: «أَبُوكَ فُلَانٌ»، فَنَزَلَتْ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِنْ تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ} [المائدة: 101].
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2359]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, akawahutubia akasema:
"Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana" Akasema: Haikuwahi kutokea kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, akasema: Wakafunika nyuso zao huku wakitoa sauti za kugugumia (kwa vilio), anasema: Akasimama Omari akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii, anasema: akasimama yule bwana akasema: Ni nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni" [Al-Maaida: 101].
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2359]
Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, nalo ni kwamba wao walimzidishia maswali, akakasirika, na akawahutubia, akasema: Nimeonyeshwa Pepo na Moto; sikuwahi kuona kheri nyingi kuliko nilizoziona siku ya leo Peponi, wala shari kubwa kuliko nilizoziona siku hiyo Motoni, na lau kama mngeliona nilichokiona, na mkajua ninachokijua katika yale niliyoyaona siku ya leo na kabla ya leo, basi mngelihuzunika huzuni kubwa, na kungepungua kucheka kwenu, na kungezidi kulia kwenu. Anasema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Haikuwahi kutoka kwa Maswahaba wake rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, na wakafunika vichwa vyao huku wakitoa sauti ya kunung'unika inayotoka puani kwa sababu ya kulia sana. Akasimama Omari radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii. Akasema: Akasimama yule bwana, akasema: Nani baba yangu?
Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo yakikudhihirikieni yatakuchukizeni" [Al-Ma’idah: 101].