+ -

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال:
كُنْتُ خَلْفَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمًا، فَقَالَ: «يَا غُلَامُ، إِنِّي أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ، احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلِ اللهَ، وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللهِ، وَاعْلَمْ أَنَّ الْأُمَّةَ لَوِ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ، لَمْ يَنْفَعُوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وَلَوِ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ، لَمْ يَضُرُّوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الْأَقْلَامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ».

[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2516]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema:
Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: "Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno, muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapoomba basi muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na tambua kuwa umma mzima lau wangekusanyika ili wakunufaishe kwa chochote, basi wasingelikunufaisha isipokuwa kwa kitu alicho kuandikia Mwenyezi Mungu kuwa chako, na lau kama wangelikusanyika ili wakudhuru kwa chochote, basi wasingeweza kukudhuru isipokuwa kwa kitu alichokiandika Mwenyezi Mungu dhidi yako, kalamu zimenyanyuliwa na kurasa zimekauka".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 2516]

Ufafanuzi

Anaeleza bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa yeye alipokuwa kijana mdogo alikuwa kapanda pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema kumwambia -Amani iwe juu yake-: Hakika mimi ninakufundisha vitu na mambo ambayo Mwenyezi Mungu atakunufaisha kwayo:
Muhifadhi Mwenyezi Mungu kwa kuhifadhi maamrisho yake na kuepuka makatazo yake, kiasi kwamba akukute katika utiifu na yale yenye kukuweka karibu naye, na asikukute katika maasi na madhambi, ikiwa utafanya hivyo basi malipo yako yatakuwa ni Mwenyezi Mungu kukuhifadhi kutokana na kero za Dunia na Akhera, na atakunusuru katika mambo yako magumu mahala popote utakapoelekea.
Na ukitaka kuomba jambo, basi usimuombe ila Mwenyezi Mungu kwani Yeye pekee ndiye mwenye kuwajibu waombaji.
Na ukitaka msaada basi usiutake ila kwa Mwenyezi Mungu.
Na uwe na yakini kuwa hutopata manufaa yoyote hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukunufaisha, isipokuwa kwa kile alichokiandika Mwenyezi Mungu kwako, na wala hutopata madhara hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukudhuru, isipokuwa kwa lile alilolikadiria Mwenyezi Mungu juu yako.
Na kuwa jambo hili kashaliandika Mwenyezi Mungu Mtukufu na akalikadiria kulingana na namna hekima na elimu yake zilivyopelekea, na hakuna kubadilishwa yale aliyoyaandika Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Umuhimu wa kuwafundisha vijana na watoto wadogo mambo ya dini kuanzia Tauhidi na adabu na mengineyo.
  2. Malipo huenda sawa na matendo.
  3. Amri ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kutawakali kwake bila kumtegemea asiyekuwa yeye, na yeye ndiye msaidizi bora.
  4. Kuamini maamuzi na mipango ya Mwenyezi Mungu na kuridhika nayo, nakuwa Mwenyezi Mungu amekwisha kadiria kila kitu.
  5. Atakayetelekeza amri ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu naye humtelekeza na humnyima ulinzi.