عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى لِأَهْوَنِ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا يَوْمَ القِيَامَةِ: لَوْ أَنَّ لَكَ مَا فِي الأَرْضِ مِنْ شَيْءٍ أَكُنْتَ تَفْتَدِي بِهِ؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ، فَيَقُولُ: أَرَدْتُ مِنْكَ أَهْوَنَ مِنْ هَذَا، وَأَنْتَ فِي صُلْبِ آدَمَ: أَلّاَ تُشْرِكَ بِي شَيْئًا، فَأَبَيْتَ إِلَّا أَنْ تُشْرِكَ بِي».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6557]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
“Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama: Je, mngekuwa na kitu chochote katika ardhi mngejikomboa nacho? Basi watasema: Ndio, atasema: Nilikutakeni jambo jepesi zaidi kuliko hili, nanyi mkiwa katika mgongo wa Adam: yakuwa msinishirikishe na chochote, mkakataa isipokuwa kunishirikisha na chochote".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6557]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu ambao watateswa kidogo na Moto wa Jahannam baada ya kuingia humo: Lau mngekuwa na dunia na vyote vilivyomo ndani yake, mngeweza kujikomboa kutokana na mateso haya? Watasema: Ndio, Basi Mwenyezi Mungu atasema: Nilikutaka na nikakuamrisheni jambo jepesi kuliko hilo, ilipo chukuliwa ahadi kwenu mkiwa katika mgongo wa Adam, ya kwamba msinishirikishe na chochote. Nilipowatoa katika dunia hii mlikataa kufanya chochote isipokuwa ushirikina.