عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيَّ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ:
بَعَثَ عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ اليَمَنِ بِذُهَيْبَةٍ فِي أَدِيمٍ مَقْرُوظٍ، لَمْ تُحَصَّلْ مِنْ تُرَابِهَا، قَالَ: فَقَسَمَهَا بَيْنَ أَرْبَعَةِ نَفَرٍ، بَيْنَ عُيَيْنَةَ بْنِ بَدْرٍ وَأَقْرَعَ بْنِ حابِسٍ وَزَيْدِ الخَيْلِ، وَالرَّابِعُ: إِمَّا عَلْقَمَةُ وَإِمَّا عَامِرُ بْنُ الطُّفَيْلِ، فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِهِ: كُنَّا نَحْنُ أَحَقَّ بِهَذَا مِنْ هَؤُلاَءِ، قَالَ: فَبَلَغَ ذَلِكَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «أَلاَ تَأْمَنُونِي وَأَنَا أَمِينُ مَنْ فِي السَّمَاءِ، يَأْتِينِي خَبَرُ السَّمَاءِ صَبَاحًا وَمَسَاءً»، قَالَ: فَقَامَ رَجُلٌ غَائِرُ العَيْنَيْنِ، مُشْرِفُ الوَجْنَتَيْنِ، نَاشِزُ الجَبْهَةِ، كَثُّ اللِّحْيَةِ، مَحْلُوقُ الرَّأْسِ، مُشَمَّرُ الإِزَارِ، فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ اتَّقِ اللَّهَ، قَالَ: «وَيْلَكَ، أَوَلَسْتُ أَحَقَّ أَهْلِ الأَرْضِ أَنْ يَتَّقِيَ اللَّهَ» قَالَ: ثُمَّ وَلَّى الرَّجُلُ، قَالَ خَالِدُ بْنُ الوَلِيدِ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلاَ أَضْرِبُ عُنُقَهُ؟ قَالَ: «لاَ، لَعَلَّهُ أَنْ يَكُونَ يُصَلِّي» فَقَالَ خَالِدٌ: وَكَمْ مِنْ مُصَلٍّ يَقُولُ بِلِسَانِهِ مَا لَيْسَ فِي قَلْبِهِ، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي لَمْ أُومَرْ أَنْ أَنْقُبَ عَنْ قُلُوبِ النَّاسِ وَلاَ أَشُقَّ بُطُونَهُمْ» قَالَ: ثُمَّ نَظَرَ إِلَيْهِ وَهُوَ مُقَفٍّ، فَقَالَ: «إِنَّهُ يَخْرُجُ مِنْ ضِئْضِئِ هَذَا قَوْمٌ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ رَطْبًا، لاَ يُجَاوِزُ حَنَاجِرَهُمْ، يَمْرُقُونَ مِنَ الدِّينِ كَمَا يَمْرُقُ السَّهْمُ مِنَ الرَّمِيَّةِ»، وَأَظُنُّهُ قَالَ: «لَئِنْ أَدْرَكْتُهُمْ لَأَقْتُلَنَّهُمْ قَتْلَ ثَمُودَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4351]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Alituma Dhahabu Ally bin Abii Twalib kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokea Yemen, ikiwa ndani ya kipande cha ngozi iliyochubuliwa, ambayo haijapembuliwa kutoka katika udongo wake, akasema: Akaigawa baina ya watu wanne, kati ya Uyaina bin Badri, na Aqrau bin Haabisi, na Zaidul Khairi, na wa nne alikuwa kati ya Alqama au Aamiri bin Tufail, akasema: Likamfikia hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Hivi hamna imani na mimi hali yakuwa mimi ni muaminiwa wa yule aliyeko mbinguni, zinanijia habari za mbingu asubuhi na jioni" Anasema: Akasimama bwana mmoja mwenye macho yaliyotumbukia ndani, mwenye uso uliokunjamana na mwenye paji la uso lililotokeza, mwenye ndevu nyingi, mwenye kipara, aliyekunja kikoi chake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mche Mwenyezi Mungu. Akasema: "Koma! Hivi kwani mimi si mtu ninayestahiki zaidi kumcha Mwenyezi Mungu katika watu wa ardhini" Anasema msimulizi: Kisha yule bwana akaondoka. Akasema Khalidi bin Walidi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi ni kwa nini nisikate kichwa chake? Akasema: "Hapana, huenda akawa anaswali" Akasema Khalidi: Na ni watu wangapi wanaoswali wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwa mioyoni mwao?, Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi sikuamrishwa kutoboa nyoyo za watu, wala kupasua matumbo yao" Anasema: Kisha akamtazama akiwa kampa kisogo, akasema: "Hakika watatoka katika kizazi cha huyu bwana watu wanaosoma kitabu cha Mwenyezi Mungu kikiwa kibichi (kwa uhodari), lakini hakivuki shingo zao, wanatoka katika dini kama mshale unavyotoka katika upinde", na ninadhani pia alisema: "Ikiwa nitakuwa hai nikawapata, basi nitawaua kifo cha Thamudi".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4351]
Aliagiza Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kipande cha dhahabu kutoka Yemen, kikiwa katika ngozi iliyolowekwa na kukwanguliwa, na dhahabu ilikuwa haijapembuliwa kutoka katika udongo wake, akasema: Akaigawanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya watu wanne: Uyaina bin Badri Al-Fazaari, na Aqrau bin Haabisi Al-Handhwali, na Zaidul-Khaili Al-Nab-haani, na Alqama bin Ulaatha Al-Aamiry, bwana moja katika Maswahaba zake akasema: Sisi ndiyo tulikuwa na haki zaidi kuliko hawa, akasema: Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Hivi hamna imani na mimi hali yakuwa mimi ni muaminiwa wa aliyembinguni, zinanijia mimi habari za mbinguni asubuhi na jioni." Anasema: Akasimama mtu mmoja mwenye macho madogo, yaliyoingia ndani ya kope zake, mwenye mashavu makubwa, na mwenye paji refu lililotokeza, na ndevu zake ni nyingi lakini si ndefu, mwenye kipara, na kikoi chake kiko juu upande wa chini wa mwili wake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mche Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Koma!, hivi kwani mimi si mtu mwenye haki zaidi kwa viumbe wa ardhini kumuogopa Allah?!". Anasema: Kisha yule bwana akaondoka, akasema Khalidi bin Walidi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi ni kwa nini nisikate kichwa chake? Akasema: Hapana, huenda akawa anaswali, Khalidi akasema: Kwani wa ngapi wanaoswali lakini wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwa mioyoni mwao?, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mimi sikuamrishwa kutoboa nyoyo ili kutazama yaliyoko ndani ya nyoyo za watu, wala kupasua matumbo yao; bali nimeamrishwa nichukue yale yanayodhihiri katika mambo yao, akasema: Kisha akamtazama yule akiwa kampa kisogo, akasema: Hakika watatoka watu kutoka katika kizazi cha huyu au kabila lake, watu mahiri katika kusoma kitabu cha Allah, tena kwa sauti nzuri, ndimi zao saa zote ni mbichi kwa wingi wa kukisoma kwake, lakini Qur'ani haivuki koo zao nyoyo zao zikaifahamu ikazitengeneza, na wala Mwenyezi Mungu hainyanyui wala haikubali Qur'ani hiyo wasomayo, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu kama utokavyo mshale katika upinde, kwa kasi na wepesi. Na ninadhani alisema: Nikifika kuwa hai wakati wanatoka dhidi ya waislamu kwa mapanga nitawaua kifo kibaya kama kaumu ya Thamudi.