عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: إِذَا حَدَّثْتُكُمْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَأَنْ أَخِرَّ مِنَ السَّمَاءِ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَكْذِبَ عَلَيْهِ، وَإِذَا حَدَّثْتُكُمْ فِيمَا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ فَإِنَّ الحَرْبَ خَدْعَةٌ، سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«يَأْتِي فِي آخِرِ الزَّمَانِ قَوْمٌ حُدَثَاءُ الأَسْنَانِ سُفَهَاءُ الأَحْلاَمِ، يَقُولُونَ مِنْ خَيْرِ قَوْلِ البَرِيَّةِ، يَمْرُقُونَ مِنَ الإِسْلاَمِ كَمَا يَمْرُقُ السَّهْمُ مِنَ الرَّمِيَّةِ، لاَ يُجَاوِزُ إِيمَانُهُمْ حَنَاجِرَهُمْ، فَأَيْنَمَا لَقِيتُمُوهُمْ فَاقْتُلُوهُمْ، فَإِنَّ قَتْلَهُمْ أَجْرٌ لِمَنْ قَتَلَهُمْ يَوْمَ القِيَامَةِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3611]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake: Nikikuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi kuporomoka kutoka mbinguni ni bora zaidi kwangu kuliko kumsemea uongo, na nikikuhadithieni katika yale yaliko baina yangu na nyinyi basi tambueni kuwa vita ni ulaghai (uongo), nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu, watazungumza maneno mazuri kuliko maneno ya viumbe wote, (lakini) wanatoka katika Uislamu kama unavyotoka mshale katika upinde, imani yao haitovuka koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo siku ya Kiyama kwa atakayewaua".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3611]
Ameeleza kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba, mtakaponisikia ninakuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi hakika mimi sifichi wala sibuni, wala sifuniki haki, bali ninaweka wazi, na kuanguka kwangu kutoka juu mbinguni ni rahisi na ni bora sana kwangu kuliko kusimulia jambo la uongo nikasema kuwa limetoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na nikisimulia mambo yalio kati yangu mimi na watu wengine, basi vita ni udanganyifu, hapo ninaweza kusema kwa mafumbo au kubuni au kuficha, kwani nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Watatokea katika zama za mwisho vijana wenye umri mdogo, wasiojitambua (madhaifu wa akili) watakuwa wakisema maneno kutoka ndani ya Qur'ani na wakiisoma kwa wingi, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu na wakivuka mipaka yake, kama mshale utokavyo katika upinde, Imani yao haivuki koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo kwa atakayewauwa, siku ya Kiyama.