عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَيْسَ الْمُؤْمِنُ بِالطَّعَّانِ وَلاَ اللَّعَّانِ وَلاَ الفَاحِشِ وَلاَ البَذِيءِ».
[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 1977]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [سنن الترمذي - 1977]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa si katika mambo ya muumini mwenye imani kamili kuwa mtoa aibu za watu katika nasaba zao, wala mwingi wa matusi na laana, wala muovu wa vitendo na kauli ambaye hana haya.