عَنِ المُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لاَ يَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ، حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ ظَاهِرُونَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 7311]
المزيــد ...
Kutoka kwa Mughira bin Shuuba -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu nao wakiwa katika kudhihiri huko".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 7311]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa hawatoacha watu katika Umma wake kuendelea kuwepo, na kuwashinda wanaopingana nao, na hilo litaendelea mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu kwa kuchukuliwa roho zao mwisho wa zama za dunia kabla ya kusimama kwa Kiyama.