عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«خَيْرُكُمْ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ» قَالَ عِمْرَانُ: لاَ أَدْرِي أَذَكَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعْدُ قَرْنَيْنِ أَوْ ثَلاَثَةً، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ بَعْدَكُمْ قَوْمًا يَخُونُونَ وَلاَ يُؤْتَمَنُونَ، وَيَشْهَدُونَ وَلاَ يُسْتَشْهَدُونَ، وَيَنْذِرُونَ وَلاَ يَفُونَ، وَيَظْهَرُ فِيهِمُ السِّمَنُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2651]
المزيــد ...
Kutoka kwa Imrani bin Huswain radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Karne bora ni karne yangu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata" Amesema Imrani: Sijui alitaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadaye karne mbili au tatu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika baada yenu kutakuja watu wanaofanya hiyana na wala hawaaminiwi, na wanatoa ushahidi na wala hawatakwi ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na utadhihiri kwao unene".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2651]
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa tabaka bora la watu waliokusanyika katika zama moja ni tabaka ambalo yuko ndani yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Maswahaba zake, kisha wale wanaowafuata katika waumini wale waliowapata Maswahaba na hawakumpata Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha wale wanaowafuata nao ni wafuasi wa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapata wasi wasi swahaba katika kutaja wale wanaowafuata kwa karne ya nne. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika baada yao kuna kizazi (kaumu) watafanya hiyana na wala watu hawatowaamini, na watatoa ushahidi kabla ya kutakwa kutoa ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na wanachupa mipaka katika ulaji na unywaji mpaka unadhihiri kwao unene.