عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أَلاَ أُحَدِّثُكُمْ حَدِيثًا عَنِ الدَّجَّالِ، مَا حَدَّثَ بِهِ نَبِيٌّ قَوْمَهُ؟ إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّهُ يَجِيءُ مَعَهُ بِمِثَالِ الجَنَّةِ وَالنَّارِ، فَالَّتِي يَقُولُ إِنَّهَا الجَنَّةُ هِيَ النَّارُ، وَإِنِّي أُنْذِرُكُمْ كَمَا أَنْذَرَ بِهِ نُوحٌ قَوْمَهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3338]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto, na hakika mimi ninakutahadharisheni kama alivyo watahadharisha Nabii Nuhu watu wake".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3338]
Anawaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake kuhusu Dajali, sifa zake, na dalili zake, kwa mambo ambayo hakuna Nabii yeyote aliyetangulia kuyasimulia kabla yake, miongoni mwa hayo ni:
Chongo wa jicho.
Na Mwenyezi Mungu kampa kitu mfano wa Pepo na Moto, kulingana na mtazamo wa macho.
Bali Pepo yake ni Moto na Moto wake ni Pepo, mwenye kumtii atamuingiza katika Pepo hii kama watu wanavyoiona, lakini uhalisia wake ni Moto wenye kuunguza, na atakayemuasi atamuingiza Motoni kama watu wanavyouona, lakini kwa uhalisia ni Pepo nzuri. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akatuonya dhidi ya fitina yake kama vile Nuhu alivyowaonya watu wake kuhusu hilo.