عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«أَسْرِعُوا بِالْجِنَازَةِ، فَإِنْ تَكُ صَالِحَةً فَخَيْرٌ تُقَدِّمُونَهَا، وَإِنْ يَكُ سِوَى ذَلِكَ، فَشَرٌّ تَضَعُونَهُ عَنْ رِقَابِكُمْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1315]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1315]
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwenda mbio kuliandaa jeneza na kuliswalia na kuzika; jeneza likiwa jema basi mnaliwahisha kwenda katika kheri miongoni mwa neema za kaburi, na likiwa kinyuume na hivyo, basi hiyo ni shari mnaiweka katika shingo zenu.