عن مَرْثَد الغَنَويّ رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال:«لا تصلُّوا إلى القُبُور، ولا تجلِسُوا عليها».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...
Kutoka kwa Marthadi Al-Ghanawiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye Amesema: "Msiswali makaburini, wala msiyakalie makaburi".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
Amekataza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuswali katika makaburi, yaani kaburi liwe upande wa mwenye kuswali, na vile vile amekataza kukaa juu ya makaburi, na katika hilo ni kuyadhalilisha kwa kuyakanyaga kwa miguu, au kukidhi haja juu yake, na yote hayo ni haramu.