+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لاَ يُصَلِّي أَحَدُكُمْ فِي الثَّوْبِ الوَاحِدِ لَيْسَ عَلَى عَاتِقَيْهِ شَيْءٌ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 359]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 359]

Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali katika nguo moja kutoyaacha wazi mabega yake na shingo yake kiasi kwamba haweki chochote chenye kumsitiri; kwa sababu mabega mawili hata kama si uchi; ila kuyasitiri yanawezekana wakati wa kusitiri uchi, na ni jambo lililo karibu na kumheshimu na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusimama mbele yake katika swala.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية النيبالية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Inafaa kuswali katika nguo moja ikiwa itasitiri sehemu za wajibu kusitiriwa.
  2. Inafaa kuswali katika nguo mbili, moja inasitiri juu ya mwili, na nyingine inasitiri chini yake.
  3. Inapendeza na ni sunna mwenye kuswali awe katika muonekano mzuri.
  4. uwajibu wa kufunika mabega mawili au moja ndani ya swala, akiweza kufanya hivyo, na imesemekana kuwa katazo ni la kujitakasa (mbele ya Mwenyezi Mungu).
  5. Uchache wa yale waliyoyamiliki Maswahaba katika mali, mpaka utakuta mmoja wao hamiliki nguo mbili.
  6. Amesema Imam Nawawi katika maana ya hadithi: Hekima yake nikuwa akijifunga chini na kukawa juu ya mabega yake hakuna kitu basi hatosalimika na kutofunuka uchi wake, tofauti na ambavyo atakaiweka sehemu ya nguo juu ya bega lake, na ni kwa sababu anaweza kuhitaji kuishika kwa mkono wake au mikono yake akashughulishwa na hilo, na ikampita sunna ya kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto chini ya kifua chake, na kuinyanyua kwake pale ambapo ni sheria kuinyanyua, na mengineyo, kwa sababu ndani yake kuna kuacha kusitiri juu ya mwili na sehemu ya pambo, na alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Chukueni pambo lenu katika kila msikiti" [Al-Araf: 31].