عن علي رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«رُفِعَ الْقَلَمُ عن ثلاثة: عن النائم حتى يَسْتَيْقِظَ، وعن الصبي حتى يَحْتَلِمَ، وعن المجنون حتى يَعْقِلَ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في الكبرى وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 4403]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 4403]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kubeba wajibu ni lazima kwa mwanadam isipokuwa hawa watatu:
Mtoto mdogo mpaka akue na abalehe.
Na kwa mwendawazimu aliyepoteza akili mpaka akili irudi.
Na kwa aliyelala mpaka aamke.
Kubeba wajibu kumeondolewa kwao, na kutenda kwao madhambi hakuandikwi, lakini mtoto huandikiwa kheri anapofanya, isipokuwa mwendawazimu na aliyelala; kwa sababu wote hawa wako katika kundi la mtu asiyekubalika ibada yake kwa kupoteza hisia.