عَنْ زِيَادِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه قَالَ:
ذَكَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْئًا، فَقَالَ: «ذَاكَ عِنْدَ أَوَانِ ذَهَابِ الْعِلْمِ» قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَكَيْفَ يَذْهَبُ الْعِلْمُ، وَنَحْنُ نَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَنُقْرِئُهُ أَبْنَاءَنَا وَيُقْرِئُهُ أَبْنَاؤُنَا أَبْنَاءَهُمْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ؟ قَالَ: «ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ زِيَادُ، إِنْ كُنْتُ لَأُرَاكَ مِنْ أَفْقَهِ رَجُلٍ بِالْمَدِينَةِ، أَوَلَيْسَ هَذِهِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى يَقْرَؤونَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ، لَا يَعْمَلُونَ بِشَيْءٍ مِمَّا فِيهِمَا؟!».

[صحيح لغيره] - [رواه ابن ماجه]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Ziyaad Bin Labiid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu" Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni vipi inaondoka elimu, na hali yakuwa sisi tunaisoma Qur'ani na tunawasomesha watoto wetu na watoto wetu wanawasomesha watoto wao mpaka siku ya Kiyama? Akasema: "Akukose mama yako ewe Ziadi ikiwa nitakuzingatia wewe ni miongoni mwa wajuzi katika mji wa Madina, hivi hawa siyo Mayahudi na Manaswara wanaisoma Taurati na Injili, na hawafanyii kazi chochote katika yale yaliyomo?!"

Ni sahihi kwa sababu ya hadithi nyingine - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amekaa kati ya Maswahaba zake, akasema: Huu ndiyo wakati ambao itaondolewa na kupokonywa elimu kutoka kwa watu, Hivyo akashangaa Ziyaad Bin Labiid Al-Answaariy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Akasema: Ni vipi itaondolewa elimu na kutupotea sisi?! Na hali yakuwa tumeisoma Qur'ani na tukaihifadhi; Namuapia Mwenyezi Mungu kuwa tutaisoma, na kuwasomesha wake zetu na watoto wetu, na wajukuu wetu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa anaona ajabu: Amekukosa mama yako ewe Ziyaad! kama ikiwa nitakuzingatia wewe ni katika wajuzi wa mji wa Madina! Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akaweka wazi kuwa kuiokosa elimu siyo kuikosa Qur'ani, bali kukosa elimu ni kuacha kuifanyia kazi, Kwa mfano hii hapa Taurati na Injili ipo kwa Mayahudi na Manaswara; na pamoja na hivyo haiwanufaishi, wala hawapati faida kutokana na makusudio yake; na faida yenyewe ni kufanyia kazi walicho jifunza.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuwepo kwa Misahafu na vitabu kwenye mikono ya watu, haviwafai pasina kuvifanyia kazi.
  2. Kuondoshwa elimu kunakuwa kwa mambo mengi, miongoni mwayo ni: Kufariki kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kufa kwa Maulamaa, na kuacha kuifanyia kazi elimu.
  3. Miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondoka elimu na kuacha kuifanyia kazi.
  4. Kuhimizwa kuifanyia kazi elimu, na hayo ndiyo makusudio.