+ -

عَنْ أَبِي مُسْلِمٍ الْخَوْلَانِيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي الْحَبِيبُ الْأَمِينُ، أَمَّا هُوَ فَحَبِيبٌ إِلَيَّ، وَأَمَّا هُوَ عِنْدِي فَأَمِينٌ، عَوْفُ بْنُ مَالِكٍ الْأَشْجَعِيُّ رضي الله عنه قَالَ:
كُنَّا عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، تِسْعَةً أَوْ ثَمَانِيَةً أَوْ سَبْعَةً، فَقَالَ: «أَلَا تُبَايِعُونَ رَسُولَ اللهِ؟» وَكُنَّا حَدِيثَ عَهْدٍ بِبَيْعَةٍ، فَقُلْنَا: قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رَسُولَ اللهِ، ثُمَّ قَالَ: «أَلَا تُبَايِعُونَ رَسُولَ اللهِ؟» فَقُلْنَا: قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رَسُولَ اللهِ، ثُمَّ قَالَ: «أَلَا تُبَايِعُونَ رَسُولَ اللهِ؟» قَالَ: فَبَسَطْنَا أَيْدِيَنَا وَقُلْنَا: قَدْ بَايَعْنَاكَ يَا رَسُولَ اللهِ، فَعَلَامَ نُبَايِعُكَ؟ قَالَ: «عَلَى أَنْ تَعْبُدُوا اللهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَالصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ، وَتُطِيعُوا -وَأَسَرَّ كَلِمَةً خَفِيَّةً- وَلَا تَسْأَلُوا النَّاسَ شَيْئًا» فَلَقَدْ رَأَيْتُ بَعْضَ أُولَئِكَ النَّفَرِ يَسْقُطُ سَوْطُ أَحَدِهِمْ، فَمَا يَسْأَلُ أَحَدًا يُنَاوِلُهُ إِيَّاهُ.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1043]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muslim Al-Khaulani, amesema: Alinihadithia kipenzi mwaminifu, ama yeye kiukweli ni kipenzi changu, na ama kiukweli kwangu ni mwaminifu, Auf Bin Maliki Al-Ashjai radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Tulikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake,inakaribia kama watu tisa au nane au saba hivi, akasema: "Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?" Na tulikuwa bado wageni katika hilo, tukasema: Tumekwisha kupa ahadi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kisha akasema: "Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?" Tukasema: tumekwisha kupa ahadi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kisha akasema: "Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?" Akasema: Tukanyoosha mikono yetu na tukasema: Tukasema: tumekwisha kupa ahadi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu,........

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1043]

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kundi la Masahaba, akawataka mara tatu mfululizo wampe ahadi ya utiifu na wampe ahadi ya kushikamana na mambo haya:
La kwanza: Kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kwa kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake, na wasimshirikishe na kitu kingine.
La pili: Kusimamisha swala tano za faradhi, katika usiku na mchana.
La tatu: Kusikia na kutii katika mambo mema kwa yule atakayesimamia majukumu ya waislamu.
La nne: Kushusha haja zao zote kwa Mwenyezi Mungu na wasiwaombe watu chochote katika haja hizo, na katika hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akashusha sauti yake.
Na hakika Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao waliyafanyia kazi yale waliyoyatolea ahadi, mpaka akasema mpokezi wa hadithi: Hakika niliwaona baadhi yao hao Masahaba unadondoka mjeledi wa mmoja wao, na hamuombi yeyote amuokotee, bali anashuka na anauchukua yeye mwenyewe.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuacha kuwaomba watu, na kujiepusha na kila kinachoitwa kuomba, na mtu kutosheka na watu hata kama itakuwa ni katika jambo jepesi.
  2. Kuomba kulikokatazwa: Ni kuomba kunakohusiana na maswala ya kidunia, hivyo kuomba elimu na mambo ya dini hakuingii hapa.
Ziada