عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال:
جَاءَ نَاسٌ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَسَأَلُوهُ: إِنَّا نَجِدُ فِي أَنْفُسِنَا مَا يَتَعَاظَمُ أَحَدُنَا أَنْ يَتَكَلَّمَ بِهِ، قَالَ: «وَقَدْ وَجَدْتُمُوهُ؟» قَالُوا: نَعَمْ، قَالَ: «ذَاكَ صَرِيحُ الْإِيمَانِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 132]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Walikuja watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi wakamuuliza: kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 132]
Lilikuja kundi la maswahaba kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na wakamuuliza kuhusiana na yanayowatokea katika nafsi zao miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanakuwa kwao ni mazito kuyasema kutokana na ubaya wake na kupenda kwao kujiepusha nayo Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: kwa hakika hiki ambacho mnakipata kwenye nafsi zenu ndiyo imani ya kweli na uhakika ambao unawapa msukumo ili kuzuia anayoyaweka shetani katika nyoyo na kuwazuieni kuyasema na kuyaona ni mazito kwenye nafsi zenu, na shetani kutoweza kuimiliki mioyo yenu, tofauti na yule ambaye ametawaliwa na shetani kwenye moyo wake akashindwa kupata chenye kumzuia kusema .