عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما:
أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَلَّمَهُ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ، فَقَالَ: مَا شَاءَ اللهُ وَشِئْتَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَجَعَلْتَنِي لِلَّهِ عَدْلًا؟ قُلْ: مَا شَاءَ اللهُ وَحْدَهُ».
[إسناده حسن] - [رواه ابن ماجه والنسائي في الكبرى وأحمد] - [السنن الكبرى للنسائي: 10759]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-:
Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
[Upokezi wake ni mzuri] - - [السنن الكبرى للنسائي - 10759]
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani zimfikie akamsemesha kuhusu jambo lake binafsi, kisha akasema: "Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe", Mtume rehema na amani zimfikie akaikemea kauli hii, na akamueleza kuwa kuunganisha matashi ya kiumbe na matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "na" ni shirki ndogo, haifai kwa muislamu kuitamka, kisha akamuelekeza katika kauli ya sawa na ya haki: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika matashi, na wala asiunganishe matashi ya yeyote kwa aina yoyote ya kiunganishi.