عَنِ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ:
«ذَاقَ طَعْمَ الْإِيمَانِ مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 34]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake, na Uislamu ndiyo dini, na Muhammad ni Mtume"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 34]
Anaeleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini mkweli katika imani yake uliyetulizana moyo wake kwa imani yake, atapata ukunjufu na wasaa na furaha ndani ya moyo wake na utam na ladha ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu endapo ataridhia kwa mambo haya matatu:
La kwanza: Akiridhika kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wake Mlezi, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayomfikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa muktadha wa ulezi, ikiwemo kugawa riziki na hali za waja, asipate upinzani kwa kitu chochote ndani ya nafsi yake, na asitafute Mola Mlezi zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
La pili: Aridhie kuwa Uislamu ndio Dini ya kweli, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayofungamana na Uislamu kama sheria na wajibu, na asipite njia nyingine isiyokuwa Uislamu.
La tatu: Aridhie kuwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake ni Mtume, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake na afurahie yote aliyokuja nayo pasina kusitasita wala kutia shaka, na asipite ila njia inayokwenda sambamba na muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake.