عَنْ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِخَمْسِ كَلِمَاتٍ، فَقَالَ:
«إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ لَا يَنَامُ، وَلَا يَنْبَغِي لَهُ أَنْ يَنَامَ، يَخْفِضُ القِسْطَ وَيَرْفَعُهُ، يُرْفَعُ إِلَيْهِ عَمَلُ اللَّيْلِ قَبْلَ عَمَلِ النَّهَارِ، وَعَمَلُ النَّهَارِ قَبْلَ عَمَلِ اللَّيْلِ، حِجَابُهُ النُّورُ -وَفِي رِوَايَةٍ: النَّارُ- لَوْ كَشَفَهُ لَأَحْرَقَتْ سُبُحَاتُ وَجْهِهِ مَا انْتَهَى إِلَيْهِ بَصَرُهُ مِنْ خَلْقِهِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 179]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa maneno matano, akasema:
"Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 179]
Alisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubia kwa Maswahaba zake kwa sentensi tano kamilifu, nazo ni: Ya kwanza: Kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka halali. Ya pili: Haiwezekani katika haki yake kulala; kulingana na ukamilifu wa usimamizi wake na uhai wake. Ya tatu: Ya kwamba Yeye Mtukufu anashusha mizani na kuinyanyua kulingana na vile vinavyopimwa miongoni mwa matendo ya waja yanayopanda kwake juu, na zinapimwa riziki zao zinazoshuka katika Ardhi, riziki ambayo ndiyo sehemu na fungu la kila kiumbe huishusha Yeye Mtukufu na kumfanya awe masikini, na huipandisha na kumfanya awe tajiri. Ya nne: Hupandishwa kwake waliyoyafanya waja usiku kabla ya mchana unaofuata baada yake, na amali zao za mchana kabla ya amali za usiku unaofuata baada yake; Malaika wanaohifadhi matendo ya waja hupanda na matendo ya usiku baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa mchana, na wanapanda na amali za mchana baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa usiku. Ya tano: Pazia lake Mtukufu linalozuia kumuona ni nuru au moto, laiti angelifunua basi mwangaza wa uso wake ungeunguza kila kitu mpaka pale linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; mwangaza wa uso wake ni nuru yake na utukufu wake na mng'ao wake. Na makadirio: Nikuwa, lau angeliondoa na kukifunua kinachozuia kumuona ambacho ni pazia, na akajitokeza wazi nuru ya uso wake ingeliunguza kila kitu mpaka linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; navyo ni viumbe vyote; kwa sababu jicho lake Aliyetakasika na kutukuka limezingira viumbe vyote.