Aina:
+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُول اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقْد آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وما يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [الأربعون النووية: 38]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi hakika nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja wangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko kile nilichomfaradhishia, na hatoacha mja wangu kuendelea kujiweka karibu yangu kwa mambo ya sunna mpaka nitampenda, nikishampenda nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analoonea, na mkono wake anaokamatia, na mguu wake anaotembelea, na akiniomba hakika nitampa, na akinitaka ulinzi hakika nitamlinda".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [الأربعون النووية - 38]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil-Qudsi ya kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alisema: Atakayemuudhi kipenzi miongoni mwa vipenzi vyangu na akamkasirisha na akamchukiza basi nitakua nimemjulisha na nimemtangazia uadui. Walii (Kipenzi): Ni muumini mchamungu, na kwa kadiri itakavyokuwa imani na uchamungu kwa mja ndivyo inavyokuwa nafasi yake ya kupendwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hajawahi kujiweka karibu Muislamu kwa jambo analolipenda zaidi Mwenyezi Mungu kuliko lile alilomfaradhishia na kumuwajibishia kama kufanya ibada na kuacha maharamisho, na hatoacha Muislamu kujiweka karibu kwa Mola wake Mlezi kwa ibada za sunna pamoja na faradhi mpaka atayapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akimpenda basi yeye huwa msimamizi wake katika viungo hivi vinne: Anamsimamia katika masikio yake, hayatosikia ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na anamsimamia katika macho yake, hatotazama ila yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu kuyatazama na kuyaridhia. Na anamsimamia katika mkono wake, hatofanya kwa mkono wake ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na atamsimamia katika mguu wake, hatokwenda ila katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, na hatokwenda mbio ila katika yale yenye kheri. Na pamoja na hayo, akimuomba Mwenyezi Mungu chochote basi Mwenyezi Mungu atampa alichoomba, anakuwa ni mtu mwenye kujibiwa dua, na akitaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu na akaomba hifadhi kwake kwa kutaka alindwe, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamlinda na kumhami na yale anayoyaogopa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Hadithi hii ni miongoni mwa yale anayayopokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Ilaahiy, nayo ni ile ambayo lafudhi yake na maana yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina umaalum kama Qur'ani ambapo Qur'ani imesifika nao tofauti na maneno mengine, ikiwemo kutumika kisomo chake kama ibada, nakuwa msafi kabla ya kusoma, na changamoto, sayansi zilizomo ndani yake, na mengine mengi.
  2. Katazo la kuwaudhi vipenzi wa Mwenyezi Mungu na himizo la kuwapenda, na kukiri ubora wao.
  3. Amri ya kuwafanyia uadui maadui wa Mwenyezi Mungu na uharamu wa kuwapenda.
  4. Atakayedai uwalii (Kupendwa na) Mwenyezi Mungu pasina kufuata sheria yake huyo ni muongo katika madai yake.
  5. Mapenzi ya Mwenyezi Mungu hupatikana kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho.
  6. Miongoni mwa sababu za mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa mja na kujibu maombi yake, ni kutekeleza mambo ya sunna baada ya kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho.
  7. Ushahidi juu ya utukufu wa mawalii (Vipenzi wa Mwenyezi Mungu) na daraja zao za juu.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai German Pashto Kiassam Albanian الأمهرية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الليتوانية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga المجرية التشيكية الموري Kiitaliano Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية الخميرية
Kuonyesha Tarjama
Aina tofauti
Ziada