Aina:
+ -

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى، قَالَ:
«إنَّ اللهَ كَتَبَ الحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ، ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا؛ كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا؛ كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ إلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ، وَإِنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا؛ كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، وَإِنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا؛ كَتَبَهَا اللهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً».

[صحيح] - [رواه البخاري ومسلم في صحيحيهما بهذه الحروف] - [الأربعون النووية: 37]
المزيــد ...

Kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika yale anayoyapokea kutoka kwa Mola wake Mlezi Aliyetukuka amesema:
"Hakika Mwenyezi Mungu aliandika mema na maovu, kisha akalibainisha hilo, basi yeyote atakayepania jema akawa hakulifanya; Mwenyezi Mungu huliandika kwake kuwa ni jema kamili, na akilipania na akalifanya; basi Mwenyezi Mungu huliandika kwake kuwa ni mema kumi mpaka ziada mia saba mpaka nyongeza nyingi zaidi, na akipania baya akawa hakulifanya; Mwenyezi Mungu huliandika kwake kuwa ni jema moja kamili, na akikusudia na akalifanya; basi Mwenyezi Mungu huliandika kuwa ni ovu moja".

[Sahihi] - [رواه البخاري ومسلم في صحيحيهما بهذه الحروف] - [الأربعون النووية - 37]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu amepanga mema na maovu, kisha akawabainishia Malaika wawili ni namna gani watayaandika:
Atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya jema basi litaandikwa kwake jema moja, hata kama hatolifanya, na ikiwa atalifanya basi hulipwa mara dufu kwa mara kumi mfano wake, mpaka ziada ya mia saba, mpaka ziada nyingi zaidi, na ziada huendana na yale yaliyoko moyoni kwanzia Ikhlaswi (kutakasa nia) na kuwanufaisha wengine, n.k.
Na atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya uovu kisha akauacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huanidikiwa jema moja, na ikiwa atauacha kwa sababu ya kukosa muda wa kuufanya na akiwa hajafanya sababu za kuuendea, hatoandikiwa chochote, na akiuacha kwa kushindwa huandikwa nia yake pekee, na ikiwa ataufanya litaandikwa kwa ovu moja.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya Umma huu katika kuzidishiwa mema na kuandikwa kwake, na kutozidishwa maovu.
  2. Umuhimu wa nia katika amali zote na athari yake.
  3. Fadhila za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- na upole wake na ihisani yake nikuwa mwenye kudhamiria jema na akawa hakulifanya Allah huliandika jema kamili.
  4. ____
  5. ____
  6. ____
  7. ____
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai German Pashto Kiassam Albanian الأمهرية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga المجرية التشيكية الموري الولوف Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية الخميرية
Kuonyesha Tarjama
Aina tofauti
Ziada