عَنْ عَبْدَ اللهِ بْنِ عَمْرٍو رَضيَ اللهُ عَنْهُمَا يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ لَقِيَ اللهَ لَا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا لَمْ تَضُرَّهُ مَعَهُ خَطِيئَةٌ، وَمَنْ مَاتَ وَهُوَ يُشْرِكُ بِهِ لَمْ يَنْفَعْهُ مَعَهُ حَسَنَةٌ».
[صحيح] - [رواه أحمد] - [مسند أحمد: 6586]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali yakuwa hamshirikishi na chochote halitomdhuru dhambi lolote kwa hilo, na atakayekufa na hali yakuwa anamshirikisha, basi hakuna jema litakalomnufaisha".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Ahmad] - [مسند أحمد - 6586]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekufa na akakutana na Mwenyezi Mungu akiwa na tauhidi hamshirikishi na chochote basi huyo ni katika watu wa Peponi, hata kama akiadhibiwa kwa dhambi motoni, na atakayekufa huku akimshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote hakuna jema lolote litakalomnufaisha; na Pepo kwake ni haramu.