عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه مرفوعاً: "الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، وما منا إلا، ولكنَّ الله يُذْهِبُهُ بالتوكل". (وما منا إلا، ولكنَّ الله يُذْهِبُهُ بالتوكل) من قول ابن مسعود وليس مرفوعًا.
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mikosi ya ndege ni shirki, na hakuna yeyote miongoni mwetu ispokuwa (ana chembe ya hilo), lakini Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea" (Na hakuna yeyote miongoni mwetu, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea) Hii ni katika kauli za bin Mas'udi na haijaegemezwa kwa Mtume.
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Anaeleza na anarudia kutoa habari; ili lengo lake lidumu katika nyoyo, kuwa mikosi ya ndege- nako ni kuamini mikosi ambako kuna mzuia mtu kutolifanya jambo au kulifanya, hii ni ushirikina; kwasababu ya yale yaliyomo miongoni mwa, moyo kuambatana na asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu. Na amesema bin Mas'udi: Na hakuna yeyote miongoni mwetu ila kumeingia katika moyo wake kitu katika imani ya mikosi, lakini Mwenyezi Mungu anaiondoa imani hii ya mikosi kwa kumtegemea na kuegemea kwake, Na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi- Hii imekuja katika njia ya kuonyesha unyenyekevu na kuonyesha kupitiliza kwa jambo lililotajwa, pamoja na hivyo kumebainishwa tiba litakapotokea hilo.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama