عن طارق بن أشيم الأشجعي رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَكَفَرَ بِمَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللهِ حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ، وَحِسَابُهُ عَلَى اللهِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 23]
المزيــد ...
Kutoka kwa Twariki bin Ashiyam Al-Ashjai Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Atakayesema: Laa ilaah illa llaah, na akayapinga yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu itakuwa haramu mali yake na damu yake, na hesabu yake itakuwa juu ya Allah".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 23]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema na akashuhudia kwa ulimi wake yakuwa "Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu", Yaani: Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na akayakanusha yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na akajitenga na dini zote isipokuwa Uislamu, itakuwa haramu mali yake na damu yake kwa muislamu, hatumiliki isipokuwa dhahiri katika matendo yake, hapokonywi mali yake na wala haimwagwi damu yake, isipokuwa atakapofanya uhalifu au jinai linalopelekea hivyo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu.
Na Allah atasimamia hesabu yake siku ya Kiyama, akiwa ni mkweli atamlipa, na akiwa mnafiki atamuadhibu.