عن أبي بشير الأنصاري رضي الله عنه "أنه كان مع رسول الله صلى الله عليه وسلم في بعض أسفاره، فأرسل رسولا أن لا يَبْقَيَنَّ في رقبة بَعِيرٍ قِلادَةٌ من وَتَرٍ (أو قلادة) إلا قطعت".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abii Bashir Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-"Yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika baadhi ya safari zake, akatuma mjumbe asibakishe katika shingo ya mnyama chochote kinachotundikwa ispokuwa kikatwe".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Nikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alituma katika baadhi ya safari zake mwenye kutangaza kwa watu kuondoa vinavyotundikwa ambavyo viko katika shingo za ngamia ambavyo lengo lake ni kuzuia kijicho na kuzuia maafa, kwasababu hilo ni katika shirki ambayo ni lazima kuiondoa.