+ -

عَنْ بُرَيْدَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ حَلَفَ بِالْأَمَانَةِ فَلَيْسَ مِنَّا».

[صحيح] - [رواه أبو داود وأحمد] - [سنن أبي داود: 3253]
المزيــد ...

Kutoka kwa Buraida -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Atakayeiapia amana basi huyo si miongoni mwetu".

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 3253]

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akatahadharisha kuapia amana, nakuwa atakayefanya hivyo si miongoni mwetu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية النيبالية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kuapa kumuapia asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikiwemo: Kuiapia amana, nakuwa hilo ni katika shirki ndogo.
  2. Amana inakusanya utiifu na ibada, na kuwekeza, na pesa tasilimu, na amana.
  3. Kiapo hakikubaliki ila kwa kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kwa jina miongoni mwa majina yake au kwa sifa katika sifa zake.
  4. Amesema Al-Khattwabi: Hadithi inaonekana kuwa karaha hapa ni kwa sababu aliamrisha aape kwa Allah na kwa sifa zake, na amana si katika sifa zake, bali ni amri katika amri zake, na ni faradhi katika faradhi zake, wakakatazwa hilo kwakuwa ndani yake kuna kuifanya amana kuwa sawa na majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka na sifa zake.