عن أبي ذر الغفاري رضي الله عنه مرفوعاً: "ما الكرسي في العرش إلا كحلقة من حديد ألقيت بين ظهري فلاة من الأرض".
[صحيح] - [رواه ابن أبي شيبة في العرش، والذهبي في العلو]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Dharri Al-Ghifaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa pana".
Sahihi - Imepokelewa na Abii Shayba katika kitabuchake Al Arshi

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ya Abuu dharri kuwa kursiy pamoja na upana wake na ukubwa wake ukilinganisha na Arshi ni kama bangili la chuma lililowekwa katika jangwa la ardhi pana; Na hii inaonyesha ukubwa na utukufu wa muumbaji wake na uwezo wake uliotimia.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama