عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه:
أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَرَأَ فِي رَكْعَتَيِ الْفَجْرِ: {قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ}، وَ{قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ}.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 726]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 726]
Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akipenda kusoma katika rakaa mbili za sunna ya Alfajiri baada ya suratul-Fatiha, katika rakaa ya kwanza (Qul-yaa ayyula-kaafiruun), na katika rakaa ya pili suratul (Qul-huwallaahu ahad).