عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما:
سَأَلَ رَجُلٌ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ، مَا تَرَى فِي صَلاَةِ اللَّيْلِ، قَالَ: «مَثْنَى مَثْنَى، فَإِذَا خَشِيَ الصُّبْحَ صَلَّى وَاحِدَةً، فَأَوْتَرَتْ لَهُ مَا صَلَّى» وَإِنَّهُ كَانَ يَقُولُ: «اجْعَلُوا آخِرَ صَلاَتِكُمْ وِتْرًا» فَإِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِهِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 472]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake-:
Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili, atapochelea Alfajiri aswali rakaa moja, iwe ni witri kwa aliyo swali" na yeye alikuwa akisema: "Fanyeni swala yenu ya mwisho iwe ni witri", kwa hakika Mtume rehema na amani za Allah zimshukie kaamrisha hivyo.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 472]
Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa anahutubia juu ya Mimbari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nifundishe ni namna gani nitaswali usiku?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utaswali na kutoa salamu katika kila rakaa mbili, ukihofia kuchomoza kwa Afajiri basi swali rakaa moja itakufanyia kuwa witiri rakaa zingine ulizoswali, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiusia kuifanya swala ya mwisho ya usiku kuwa ni witiri.