عَنْ أُمِّ حَبِيبَةَ رضي الله عنها زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالت: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«مَنْ حَافَظَ عَلَى أَرْبَعِ رَكَعَاتٍ قَبْلَ الظُّهْرِ وَأَرْبَعٍ بَعْدَهَا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 428]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ummu Habiba, radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni".
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 428]
Amempa habari njema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake atakayeswali katika swala za sunna rakaa nne kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa nne baada yake, na akadumu na akazihifadhi, kuwa Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni.