عن عائشةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رضي الله عنها:
أن النبي صلى الله عليه وسلم كان لا يَدع أربعا قَبل الظهر وركعتين قبل الغَدَاة.
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 1182]
المزيــد ...
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake:
Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 1182]
Ameeleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akidumu na swala za sunna ndani ya nyumba yake na wala haziachi: Rakaa nne kwa salamu mbili kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri.