عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا شَكَّ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ، فَلَمْ يَدْرِ كَمْ صَلَّى ثَلَاثًا أَمْ أَرْبَعًا، فَلْيَطْرَحِ الشَّكَّ، وَلْيَبْنِ عَلَى مَا اسْتَيْقَنَ، ثُمَّ يَسْجُدُ سَجْدَتَيْنِ قَبْلَ أَنْ يُسَلِّمَ، فَإِنْ كَانَ صَلَّى خَمْسًا شَفَعْنَ لَهُ صَلَاتَهُ، وَإِنْ كَانَ صَلَّى إِتْمَامًا لِأَرْبَعٍ كَانَتَا تَرْغِيمًا لِلشَّيْطَانِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 571]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapopata shaka mmoja wenu katika swala yake, akawa hajui kaswali rakaa ngapi tatu au nne? Basi aachane na shaka na ajenge yakini (uhakika), kisha atasujudu sijida mbili kabla hajatoa salamu, ikiwa atakuwa kaswali rakaa tano basi zitamtetea katika swala yake, na kama aliswali kukamilisha nne; basi hiyo itakuwa ni kumvunja moyo shetani."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 571]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ikiwa mwenye kuswali atasita katika swala yake na akashindwa kujua ameswali rakaa ngapi, tatu au nne? Hebu aondoe idadi iliyozidi yenye shaka na asiihesabu; tatu ndiyo ana uhakika nazo, basi ataswali rakaa ya nne, kisha atasujudu sijida mbili kabla ya kutoa salamu.
Ikiwa aliswali nne kweli; basi zitakuwa tano kwa kuongeza rakaa moja, na sijida mbili za kusahau zitakuwa ni mbadala wa rakaa moja, basi idadi itakuwa ni shufa si witiri, na ikiwa kaswali rakaa nne kwa rakaa iliyozidi; basi atakuwa katekeleza wajibu wake pasina kuongeza wala kupunguza.
Sijida mbili za kusahau zilikuwa ni kumdhalilisha Shetani na kumshinda, na kumrudisha akiwa kafedheheka, na kashindwa kufikia lengo lake; Kwa sababu alimvurugia swala yake, na akataka kuiharibu, na ikakamilika swala ya mwanadamu alipotekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kusujudu, sijida ambayo Ibilisi aliasi, alipokataa kumtii Mwenyezi Mungu kwa kumsujudia Adamu.