عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ:
كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَغْسِلُ، أَوْ كَانَ يَغْتَسِلُ، بِالصَّاعِ إِلَى خَمْسَةِ أَمْدَادٍ، وَيَتَوَضَّأُ بِالْمُدِّ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 201]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiosha, au akioga, kwa kibaba kimoja mpaka vibaba vitano, na anatawadha kwa kibaba kimoja.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 201]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga janaba kwa kibaba kimoja mpaka vitano, na alikuwa akitawadha kwa kibaba kimoja. Na kibaba ujazo wake ni: mud nne, na mud moja ni: kiasi cha kujaza kiganja cha mtu mwenye mwili wa wastani.