عن عَبْدُ الله بن عمر رضي الله عنهما «أَنَّ امْرَأَةً وُجِدَتْ فِي بَعْضِ مَغَازِي النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم مَقْتُولَةً، فَأَنْكَرَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم قَتْلَ النِّسَاءِ، وَالصِّبْيَانِ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- "Yakwamba mwanamke mmoja alipatikana katika baadhi ya vita vya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa kauwawa, akakemea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuuwa wanawake, na watoto wadogo".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Kukemea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuuwa wanawake na watoto inaonyesha uharamu wa kuwauwa, na kauli yake katika baadhi ya hadithi zilizokuja katika maana hii: (Hakuwa huyu ni mwenye kupigana) ni angalizo juu ya sababu ya kukataza kuwauwa wanawake; kwasababu mara nyingi wao sio wenyekupigana, hata kama katika baadhi yao kuna shari na ushujaa, lakini hukumu imewekwa kwa wengi, atakayepigana atapigwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo
Kuonyesha Tarjama