عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه قال: «سُئِلَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم عَنْ الرَّجُلِ: يُقَاتِلُ شَجَاعَةً، وَيُقَاتِلُ حَمِيَّةً، وَيُقَاتِلُ رِيَاءً، أَيُّ ذَلِكَ فِي سَبِيلِ الله؟ فَقَالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : مَنْ قَاتَلَ لِتَكُونَ كَلِمَةُ الله هِيَ الْعُلْيَا، فَهُوَ فِي سَبِيلِ الله».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mtu: Anapigana kwaajili ya ushujaa, na anapigana kwaajili ya hamasa, na anapigana kwaajili ya kujionyesha, ni yupi kati ya hao yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayepigana ili liwe neno la Mwenyezi Mungu ndio la juu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alimuuliza mtu mmoja Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mtu anayewapiga vita maadui wa dini, lakini kinachompelekea kupigana ni kuonyesha ushujaa na ujasiri mbele za watu. Na kuhusu mtu anayepigana kwa kuhami watu wake, au nchi yake. Na anapigana mtu wa tatu kwa kujionyesha mbele ya macho ya watu kuwa yeye ni katika wapiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu wanaostahiki kusifiwa na kutukuzwa. Ni yupi anayepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya hawa watatu? Akajibu Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kwa ibara fupi zaidi na yenye maana pana, Nayo ni: kuwa atakayepigana ili liwe neno la Mwenyezi Mungu ndio la juu, basi huyo ndio yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu, na asiyekuwa huyu basi hayuko katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwakuwa amepigana kwa lengo jingine. Na amali zote zinaambatana na nia katika kutengemaa kwake na kuharibika kwake, na hii inajumuisha amali zote athari yake ni nia, kutengemaa na kuharibika, na dalili juu ya maana hii ni nyingi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo الدرية
Kuonyesha Tarjama