عَن أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رضي الله عنها قَالت: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ كَانَ لَهُ ذِبْحٌ يَذْبَحُهُ فَإِذَا أُهِلَّ هِلَالُ ذِي الْحِجَّةِ، فَلَا يَأْخُذَنَّ مِنْ شَعْرِهِ، وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا حَتَّى يُضَحِّيَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1977]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayeandaa mnyama kwa ajili ya kuchinja, na ukaandama mwandamo wa mwezi Dhul Hija, basi asipunguze chochote katika nywele zake wala kucha zake mpaka atakapochinja mnyama wake wa Udh-hiya"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1977]
Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayetaka kuchinja Udh-hiya asipunguze chochote katika nywele za kichwa chake au kwapa yake au sharubu zake au zinginezo, wala sehemu ya kucha za mikono yake wala miguu yake utakapoonekana mwandamo wa Dhul-Hija mpaka atakapochinja.