عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
مِنَ السُّنَّةِ إِذَا قَالَ الْمُؤَذِّنُ فِي أَذَانِ الْفَجْرِ حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، قَالَ: الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ.
[صحيح] - [رواه ابن خزيمة والدارقطني والبيهقي] - [صحيح ابن خزيمة: 386]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema:
Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi.
[Sahihi] - [رواه ابن خزيمة والدارقطني والبيهقي] - [صحيح ابن خزيمة - 386]
Ameeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa miongoni mwa mambo aliyoyakubali Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sunna zake, ni Muadhini kusema katika Adhana Alfajiri pekee, baada ya kauli yake: "Hayya a'lal falaah" asema: "Asswalaatu khairuni minan nauum" Yaani swala ni bora kuliko usingizi.