+ -

عَنْ عُقْبَةَ بْنَ عَامِرٍ الْجُهَنِيَّ رضي الله عنه قَالَ:
ثَلَاثُ سَاعَاتٍ كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْهَانَا أَنْ نُصَلِّيَ فِيهِنَّ، أَوْ أَنْ نَقْبُرَ فِيهِنَّ مَوْتَانَا: حِينَ تَطْلُعُ الشَّمْسُ بَازِغَةً حَتَّى تَرْتَفِعَ، وَحِينَ يَقُومُ قَائِمُ الظَّهِيرَةِ حَتَّى تَمِيلَ الشَّمْسُ، وَحِينَ تَضَيَّفُ الشَّمْسُ لِلْغُرُوبِ حَتَّى تَغْرُبَ.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 831]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhani radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nyakati tatu alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitukataza kuswali ndani yake, au kuzika ndani yake maiti wetu: wakati linapoanza kuchomoza jua mpaka linyanyuke, na wakati linapofika kati kati mpaka lipinde, na wakati linapoanza kuzama mpaka lizame.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 831]

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyakati tatu za mchana kutoswali ndani yake swala za sunna, au kuzikwa ndani yake maiti: Wakati wa kwanza: Wakati linapodhihiri jua kwa kuchomoza, na hii ni wakati wa mwanzo wa kuchomoza kwake mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki, na inakadiriwa kuwani robo saa takribani. Wakati wa pili: Pindi jua linapofika kati kati ya mbingu, linapokuwa halina kivuli upande wa Mashariki au Magharibi mpaka linapoondoka kutoka kati kati ya mbingu, na kikaonekena kivuli upande wa Mashariki, wakati ambapo unaanza wakati wa Adhuhuri, nao ni wakati mfupi mno; ambao ni kiasi cha dakika tano takribani. Wakati wa tatu: Linapopinda na likaanza kuzamia Magharibi mpaka lizame.

Katika Faida za Hadithi

  1. Nyakati zilizokatazwa kuswali ndani yake kama ilivyoonyesha hadithi hii na hadithi nyinginezo, nazo ni: Wa kwanza: Baada ya swala ya Alfajiri mpaka jua linapochomoza. Wa pili: Wakati wa kuchomoza jua mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki kwa mtazamo wa jicho; yaani: kiasi cha dakika kumi na tano takribani. Wa tatu: Anaposimama msimamaji wa mchana mpaka jua liondoke, na hii ni wakati ambao unakuwa hakijabakia kivuli kwa mwenye kusimama mchana, upande wa Mashariki wala Magharibi, na wameukadiria baadhi yao kuwa ni dakika tano takribani. Wa nne: Baada ya swala ya Lasiri mpaka jua lizame. Wa tano: Wakati jua linapokuwa la njano mpaka lizame.
  2. Katazo la kuswali katika nyakati hizi tano zilizokatazwa, zinaondolewa hapo swala za faradhi na swala zenye sababu.
  3. Katazo la kuchelewesha kuzika mpaka katika nyakati hizi tatu zenye muda mfinyu zilizotajwa katika hadithi, na kufaa kwake katika nyakati nyinginezo sawa iwe mchana au usiku.
  4. Hekima na maana ya kukataza kuswali ndani ya nyakati hizi: Asili ni nikuwa muislamu anajisalimisha kwa amri za Mwenyezi Mungu, na anajiepusha na makatazo yake kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, na wala haachi kuabudu mpaka aone hekima au sababu ya kuamrishwa hivyo, au kukatazwa hilo, bali anatakiwa atii, na imekuja katika hadithi zingine hekima katika hilo: Ya kwanza: Nikuwa katika wakati wa mchana kabla ya kupinduka jua Jahanamu huwashwa muwako mkali. Ya pili: Na ama hekima ya kukatazwa swala wakati wa kuchomoza jua na wakati wa kuzama kwake, ni kujifananisha na washirikina, kwani wao hulisujudia jua wakati wa kuchomoza kwake na wakati wa kuzama kwake. Ya tatu: Na ama katazo la kuswali baada ya Alfajiri mpaka kuchomoza kwa jua, na baada ya Lasiri mpaka kuzama kwake, hii ni sehemu ya kuziba njia zinazopelekea katika mabaya; mpaka kumalizike kutojifananisha na makafiri, na waislamu wasijifananishe nao katika ushirikina wao, kwani wao hulisujudia jua wakati wa kuchomoza na wakati wa kuzama kwake.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama