عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ قَتَلَ مُعَاهَدًا لَمْ يَرَحْ رَائِحَةَ الْجَنَّةِ، وَإِنَّ رِيحَهَا تُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ أَرْبَعِينَ عَامًا».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 3166]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abdillah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema:
"Atakayemuua aliyechukua ahadi ya kulindwa, hatonusa harufu ya pepo, na hakika hurufu yake hupatikana kuanzia mwendo wa miaka arobaini".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 3166]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari kubwa kwa atakayemuuwa aliyechukua ahadi ya kulindwa -Naye ni kafiri aliyeingia katika mji wa kiislamu kwa ahadi na amani- kuwa hatonusa harufu ya Pepo, na hakika harufu yake huwa kuanzia umbali wa mwendo wa miaka arobaini.