عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهُما أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم:
نَهَى عَنْ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ، وَعَنْ كُلِّ ذِي مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْرِ.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1934]
المزيــد ...
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake -:
Alikataza kula kila chenye meno ya chonge katika wanyama wanaoshambulia, na kila chenye mdomo wa chonge katika ndege.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1934]
Alikataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kula kila chenye kuwinda katika wanyama wenye kushambulia, kinachowinda kwa meno ya mbele, na akakataza kula kila ndege anayekata na kukamata kwa mdomo wake.