+ -

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ عَامَ الفَتْحِ وَهُوَ بِمَكَّةَ:
«إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الخَمْرِ، وَالمَيْتَةِ وَالخِنْزِيرِ وَالأَصْنَامِ»، فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ شُحُومَ المَيْتَةِ، فَإِنَّهَا يُطْلَى بِهَا السُّفُنُ، وَيُدْهَنُ بِهَا الجُلُودُ، وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا النَّاسُ؟ فَقَالَ: «لاَ، هُوَ حَرَامٌ»، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ: «قَاتَلَ اللَّهُ اليَهُودَ إِنَّ اللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ، ثُمَّ بَاعُوهُ، فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2236]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yao na baba yake, yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akiwa Makka:
"Hakika Allah na Mtume wake ameharamisha kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu", Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wasemaje kuhusu samli (mafuta ya wanyama), kwani hutumika kupaka boti, na hupakwa ngozi, na watu huyatumia kuwasha taa? Akasema: "Hapana, hayo ni haramu", kisha baada ya hapo akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenyezi Mungu awalaani Mayahudi, kwani Mwenyezi Mungu alipowaharamishia samli (mafuta ya wanyama) waliyayeyusha, kisha wakayauza, na wakala thamani yake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2236]

Ufafanuzi

Jabiri bin Abdillah Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema katika mwaka wa ufunguzi akiwa Makka: Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake amekataza kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je inajuzu kwetu kuuza mafuta ya wanyama waliokufa? Kwa sababu yanatumika kupaka boti (Mitumbwi), na ngozi na watu huwasha taa zao kwayo. Akasema: Hapana, kuyauza ni haramu, kisha akasema: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi, Mwenyezi Mungu alipowaharamishia mafuta ya wanyama, waliyayeyusha, kisha wakayauza na kula thamani yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Amesema Imam Nawawi: Mzoga na pombe na nguruwe: Wamekubaliana waislamu wote kuwa ni haramu kuuza chochote katika hivi.
  2. Amesema Kadhi: Hadithi hii inamaanisha kuwa kila kisichohalali kukila na kunufaika nacho basi haifai kukiuza, na wala si halali kula thamani yake, kama ilivyo katika mafuta yaliyotajwa katika hadihi
  3. Amesema bin Hajari: Mlolongo wa hadithi inaonesha kuwa ibara ya mwanzo inaguvu zaidi kwa makusudio ya kuwa kauli yake: "Ni haramu" Yaani: Kuuza na si kunufaika.
  4. Kila ujanja unaotumika kuhalalisha haramu basi ni batili.
  5. Amesema Imam Nawawi: Wamesema wanachuoni: Na katika ujumla wa uharamu wa kuuza mzoga nikuwa ni haramu kuuza maiti ya kafiri tutakapomuuwa na makafiri wakaomba kumnunua, au kutoa fidia, na imekuja katika hadithi: Yakwamba Naufal bin Abdillah Al-Makhazuumi waislamu walimuua siku ya vita vya Khandaq, makafiri wakatoa Dirham elfu kumi ili kupewa mwili wake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi hakuzichukua, na akawapa bure.