عَنْ مُعَاذٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا وَجَّهَهُ إِلَى الْيَمَنِ أَمَرَهُ أَنْ يَأْخُذَ مِنَ الْبَقَرِ مِنْ كُلِّ ثَلَاثِينَ تَبِيعًا أَوْ تَبِيعَةً، وَمِنْ كُلِّ أَرْبَعِينَ مُسِنَّةً، وَمِنْ كُلِّ حَالِمٍ -يَعْنِي مُحْتَلِمًا- دِينَارًا أَوْ عَدْلَهُ مِنَ المَعَافِرِ، ثِيَابٌ تَكُونُ بِالْيَمَنِ.
[صحيح بشواهده] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 1576]
المزيــد ...
Kutoka kwa Muadhi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamrisha achukue miongoni mwa ng'ombe katika kila thelathini ndama alianza kufuatana na ng'ombe wengine, wa kiume au kike, na katika kila arobaini mwenye miaka miwili, na kutoka kwa kila anayeishi humo asiye muislamu Dinari au kitu chenye thamani sawa na Dinari kama Maafiri, nazo ni nguo hutengenezwa Yemen.
[Ni sahihi kwa ushahidi wake] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود - 1576]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yake kwenda Yemen kwa ajili ya kuwafundisha watu na kuwafikishia ujumbe, na miongoni mwa yale aliyomuamrisha achukue kutoka kwa Waislamu zaka za ng'ombe zao katika kila ng'ombe thelathini achukue dume moja au ng'ombe aliyeanza kufuatana na wengine machungani; naye ni yule aliyetimiza mwaka moja, na katika kila ng'ombe arobaini achukue ng'ombe mkamilifu; naye ni yule aliyetimiza miaka miwili. Na achukue jizia (kodi) kutoka kwa watu wa kitabu, Mayahudi na Wakristo, kwa kila mwanaume aliyebalehe, Dinari, au kinacholingana na Dinari katika nguo za Yemen ziitwazo: Maafari.