عَنْ يحيى بنِ عُمَارةَ المَازِنِيِّ قَالَ:
شَهِدْتُ عَمْرَو بْنَ أَبِي حَسَنٍ سَأَلَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ زَيْدٍ، عَنْ وُضُوءِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَدَعَا بِتَوْرٍ مِنْ مَاءٍ، فَتَوَضَّأَ لَهُمْ وُضُوءَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَكْفَأَ عَلَى يَدِهِ مِنَ التَّوْرِ، فَغَسَلَ يَدَيْهِ ثَلاَثًا، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فِي التَّوْرِ، فَمَضْمَضَ وَاسْتَنْشَقَ وَاسْتَنْثَرَ، ثَلاَثَ غَرَفَاتٍ، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فَغَسَلَ وَجْهَهُ ثَلاَثًا، ثُمَّ غَسَلَ يَدَيْهِ مَرَّتَيْنِ إِلَى المِرْفَقَيْنِ، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فَمَسَحَ رَأْسَهُ، فَأَقْبَلَ بِهِمَا وَأَدْبَرَ مَرَّةً وَاحِدَةً، ثُمَّ غَسَلَ رِجْلَيْهِ إِلَى الكَعْبَيْنِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 186]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Yahya Bin Umaara Al-Maaziniy amesema:
Nilimshuhudia Amri Bin Abii Hasan akimuuliza Abdallah Bin Zaidi, kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha mbele yao udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamimina katika mikono yake kutoka katika bakuli, akaosha viganja vyake mara tatu, kisha akaingiza mkono wake ndani ya bakuli, akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga, kwa michoto mitatu, kisha akaingiza mkono wake akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake mara mbili mpaka katika viwiko viwili, kisha akaingiza mkono wake akafuta kichwa chake, akaanza upande wa mbele na akapeleka mpaka nyuma ya kichwa, mara moja, kisha akaosha miguu yake mpaka katika kongo mbili.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 186]
Amebainisha Abdallah Bin Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake namna ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kwa vitendo, akaomba chombo kidogo chenye maji, kwanza kabisa akaanza kuosha viganja vyake, kisha akainamisha chombo na akamimina maji akaiosha mara tatu nje ya chombo, Kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo, akachota michoto mitatu, katika kila mchoto anasukutua na anapandisha maji puani na anapenga, Kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha uso wake mara tatu, kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara mbili mbili, kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo akafuta kichwa chake kwa mikono yake akaanza na mbele ya kichwa chake mpaka akafika katika kisogo chake juu ya shingo, kisha akairejesha mpaka akafika mahali alipoanzia, kisha akaosha miguu yake pamoja na kongo mbili.