+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه:
أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ المَسْجِدَ فَدَخَلَ رَجُلٌ، فَصَلَّى، فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَرَدَّ وَقَالَ: «ارْجِعْ فَصَلِّ، فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ»، فَرَجَعَ يُصَلِّي كَمَا صَلَّى، ثُمَّ جَاءَ، فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «ارْجِعْ فَصَلِّ، فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ» ثَلاَثًا، فَقَالَ: وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالحَقِّ مَا أُحْسِنُ غَيْرَهُ، فَعَلِّمْنِي، فَقَالَ: «إِذَا قُمْتَ إِلَى الصَّلاَةِ فَكَبِّرْ، ثُمَّ اقْرَأْ مَا تَيَسَّرَ مَعَكَ مِنَ القُرْآنِ، ثُمَّ ارْكَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ رَاكِعًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَعْدِلَ قَائِمًا، ثُمَّ اسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، وَافْعَلْ ذَلِكَ فِي صَلاَتِكَ كُلِّهَا».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 757]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia msikitini kisha akaingia mtu mmoja, akaswali, kisha akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akajibu salamu, na akasema: "Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali", akarudia kuswali kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja, akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Rudi kaswali kwani wewe hujaswali" (akafanya hivyo) Mara tatu, akasema: "Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivyo, basi naomba nifundishe, akasema: "Utakaposimama katika swala basi toa takbira (sema: Allaahu Akbaru), kisha soma kiasi chepesi ulichonacho katika Qur'ani, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa, na ufanye hivyo katika swala yako yote".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 757]

Ufafanuzi

Aliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini, akaingia baada yake mtu mmoja akaswali rakaa mbili haraka haraka, na hakutulizana katika kisimamo chake na rukuu yake na sijida yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimfuatilia katika swala yake, akaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa kakaa pembezoni mwa msikiti, akamsalimia, akamjibu salamu, na akasema kumwabia: Nenda karudie swala; kwani wewe hujaswali. Akarudi na akaswali haraka kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kuwambia: Rudi kaswali; kwani wewe hujaswali, alifanya hivyo mara tatu. Yule bwana akasema: Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kufanya vizuri zaidi ya hivyo, basi nifundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utakaposimama katika swala basi toa takbira ya kuhirimia swala, kisha soma mama wa Qur'ani (Suratul-Faatiha) na kile atakachotaka Mwenyezi Mungu ukisome, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu kwa kuweka viganja vyako juu ya magoti yako na unyooshe mgongo wako na umakinike katika rukuu yako, kisha nyanyuka na unyooshe mgongo wako mpaka mifupa irudi katika viungo vyake na ulingane sawa ukiwa wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu kwa kuliweka sawa paji la uso na pua, na mikono miwili na magoti mawili na ncha za vidole vya miguu miwili juu ya ardhi, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa kati ya sijida mbili, kisha fanya hivyo katika kila rakaa ndani ya swala yako.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Nguzo hizi za swala hazidondoki kwa kusahau wala kwa ujinga, kwa dalili ya kuamrishwa mwenye kuswali kurudia, na wala hakutosheka Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kumfundisha pekee.
  2. Kutulia ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala.
  3. Amesema Nawawi: Na hapa nikuwa atakayepunguza baadhi ya wajibu za swala basi haitoswihi swala yake.
  4. Amesema Nawawi: Na ndani ya hili kuna kumhurumia mwenye kujifunza na mjinga na kuwa mpole kwake, na kumuwekea wazi maswala na kufupisha makusudio, na kufupisha katika haki zake yale ya muhimu pasina yale yenye kukamilisha, ambayo yanategemea mpaka kuyahifadhi na kuyatekeleza.
  5. Amesema Nawawi: Na hapa nikuwa Mufti akiulizwa kuhusu jambo na kukawa na jambo jingine muhimu zaidi analolihitajia muulizaji lakini hakuliulizia basi ni sunna alieleze, na hii inakuwa ni katika nasaha na si katika kuzungumza yasiyomuhusu.
  6. Fadhila za kukiri mapungufu, kwa kauli yake: "Siwezi kufanya vizuri zaidi ya hivyo, basi nifundishe".
  7. Amesema bin Hajari: Hapa kuna kuamrisha mema na kukataza maovu, na mwenye kujifunza kumuomba mwalimu amfundishe.
  8. Sunna ya kutoa salamu wakati wa kukutana, na uwajibu wa kuitikia, na kwamba inapendeza kukutana mara kwa mara hata kama muda utakaribiana, na kwamba ni lazima kuitikia kwa kila mara.