عن عبد الله بن عُمر وأبي هريرة رضي الله عنهما أنهما سمعا رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول على أعواد منبره:
«لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ الْجُمُعَاتِ أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اللهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ، ثُمَّ لَيَكُونُنَّ مِنَ الْغَافِلِينَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 865]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Omari na Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yao, ya kwamba wao walimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema akiwa juu ya Mimbari yake:
"Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu atawapiga mihuri juu ya mioyo yao, kisha kwa hakika watakuwa ni miongoni mwa walioghafilika".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 865]
Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa juu ya Mimbari yake, mwenye kuacha swala ya Ijumaa na kutohudhuria bila udhuru, kwa uvivu na uzembe, au vinginevyo Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya nyoyo zao na kuzifunika na kuziwekea kizuizi kitakachozizuia kufuata haki, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika kuzikumbuka sababu za kheri, na kinachokataa kheri ni nafsi zao wao wenyewe.