عَنْ أَبِي الْجَعْدِ الضَّمْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ، وَكَانَتْ لَهُ صُحْبَةٌ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ تَرَكَ ثَلَاثَ جُمَعٍ تَهَاوُنًا بِهَا طَبَعَ اللَّهُ عَلَى قَلْبِهِ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 1052]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abul Ja'di Adh-dhwamri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa na uswahaba, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema:
"Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake"
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 1052]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoacha swala ya Ijumaa, na kwamba mwenye kuacha swala ya Ijumaa mara tatu kwa kupuuza na uzembe pasina udhuru basi Mwenyezi Mungu atapiga na kufunika juu ya moyo wake na kizibo kinachozuia kuingia kheri yoyote ndani ya nafsi yake.