عن تميم الداري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 55]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Tamim Ad-dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
"Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 55]
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dini imesimama katika misingi ya kutakasa nia (Ikhlas) na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu, kikamilifu bila uzembe au udanganyifu.
Akaulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nasaha huwa kwa ajili ya nani? Akasema:
Kwanza: Nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha mwingine pamoja naye, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kuzitukuza amri zake, na kulingania watu katika kumuamini.
Pili: Nasaha ni kwa ajili ya kitabu cha Mwenyezi Mungu nacho ni Qur'ani Tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, nakuwa kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza, na tunakisoma ukweli wa kukisoma, na tunazifanyia kazi aya zake za wazi, na tunazikubali zenye kutatiza, na tunapinga upotoshaji wa wenye kupindisha, na tunayazingatia mawaidha yake, na kuieneza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo.
Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Tuitakidi kuwa yeye ni Mtume wa mwisho, na tumsadikishe katika yale aliyokuja nayo, na tutekeleze amri zake, na tuyaepuke makatazo yake, na tusimuabudu Allah isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tuitukuze haki yake, na tumuheshimu, na tuutangaze ujumbe wake, na tuisambaze sheria yake, na tuzikanushe tuhuma dhidi yake.
Nne: Nasaha kwa viongozi wa waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu.
Tano: Nasaha kwa waislamu: Kwa kuwafanyia wema na kuwalingania, na kuzuia maudhi dhidi yao, na kuwapendelea kheri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.