عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَا شَيْءٌ أَثْقَلُ فِي مِيزَانِ الْمُؤْمِنِ يَوْمَ القِيَامَةِ مِنْ خُلُقٍ حَسَنٍ، وَإِنَّ اللَّهَ لَيُبْغِضُ الفَاحِشَ البَذِيءَ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي] - [سنن الترمذي: 2002]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Dardai Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake Amesema:
"Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu".
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2002]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama katika kauli na matendo ni tabia njema, na hii ni kwakuwa na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi, na kutenda wema. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anamchukia mtu muovu katika kauli zake na vitendo, mwenye mdomo mchafu katika yale yanayotamkwa na ulimi wake.